Teknolojia Yetu

Xpeed imejengwa kwa teknolojia ya kisasa (Flutter & Laravel) ili kuhakikisha kasi, usalama, na urahisi kwa watumiaji wote.

Token System

Mfumo wa kipekee kwa Bodaboda. Nunua tokens za 100 Tsh kufanya kazi. Hakuna makato ya asilimia (Commission) au madeni ya wiki.

Hyper-Local Map

Ramani yetu imeundwa kutambua vichochoro na maduka ya mtaani ambayo Google Maps haioni. Tunakuunganisha na Duka la Mangi halisi.

Uthibitisho wa Picha

Kabla Rider hajaondoka dukani, lazima apige picha mzigo kupitia App. Mteja anaona picha hiyo papo hapo kwa usalama zaidi.

Lugha Yetu

App nzima imetengenezwa kwa Kiswahili fasaha. Maneno rahisi kama "Oda", "Lipa", na "Mteja" yanamfanya yeyote aweze kutumia.

Kasi ya Umeme

Algorithm yetu inatafuta Rider aliye karibu zaidi (ndani ya 2km) ili kuhakikisha mzigo wako unafika ndani ya dakika 15.

Usalama wa Data

Taarifa zako ni siri. Tunatumia teknolojia ya usalama ya hali ya juu (Encryption) kulinda namba zako za simu na miamala.